
-
- Author, Anastasiya Gribanova
- Akiripoti kutoka, Kyiv
-
Muda wa kusoma: Dakika 4
Makala hii ina maelezo ya kusikitisha. Baadhi ya majina yamebadilishwa ili kulinda utambulisho.
Kateryna hawezi kusimulia yaliyomkuta mwanawe wa kiume, Orest, bila kububujikwa na machozi. Sauti yake inasikika ikitetemeka kwa uchungu akielezea jinsi alivyopata taarifa ya mwanawe kufariki vitani katika eneo la Donetsk mashariki mwa Ukraine mwaka 2023.
Kulingana na uchunguzi rasmi uliofanywa na jeshi, alifariki kutokana na “majeraha ya kujidhuru mwenyewe”, jambo ambalo Katernya analitilia shaka.
Kateryna ameomba jina la marehemu mwanawe kutotajwa kutokana na hali ya unyanyapaa inayozunguka suala la kujitoa uhai na afya ya akili nchini Ukraine.
Orest 25, alikuwa kijana mpole aliyependa kusoma na mwenye ndoto ya kuwa mtaalamu katika maisha yake ya masomo. Macho yake mabaya yalikuwa yamemfanya kutotumikia nchi mwanzoni mwa vita, mama yake anasema.
Lakini 2023, maafisa waliokuwa wakifanya msako wa kuwasajili vijana jeshini walimsimamisha njiani. Macho yake yalikaguliwa upya na kuona kuwa anaweza kupigana. Muda mfupi baadaye, alipelekwa mstari wa mbele kama mtaalamu wa mawasiliano.
Chanzo cha picha, EPA
Ukraine imepoteza takribani wanajeshi 45,000 tangu uvamizi kamili wa Urusi mnamo 2022.
Hakuna takwimu rasmi kuhusu vifo vinavyotokana na kujitoa uhai miongoni mwa wanajeshi. Maafisa wanayaelezea kama matukio nadra. Hata hivyo watetezi wa haki za binadamu na familia zilizofiwa wanaamini mamia huenda wamefariki.
“Orest alikamatwa, hakusajiliwa kwa njia inayostahili,” Kateryna anasema kwa uchungu.
Kituo cha kuwaasajili vijana jeshini kiliiambia BBC kwamba hakikufanya makosa, kikisema kuwa hali ya kutoona vizuriil ilimfanya Orest “asiwe mkamilifu” wakati wa vita.
Mara baada ya kutumwa karibu na Chasiv Yar huko Donetsk, Orest alizidi kujitenga na kuonyesha dalili ya kukumbwa na mfadhaiko, Kateryna anakumbuka.
Bado anamuandika barua mwanawe kila siku – 650 na zinazidi kuongezeka – masikitiko yake yake yanatokana na jinsi Ukraine inaainisha kujiua kama kifo ambacho hakihusiani na vita. Familia za wale wanaojitoa uhai hazipati fidia, hakuna heshima za kijeshi na hakuna kutambuliwa kwa umma.
“Watu nchini Ukraine ni kama wamegawanginka ,” anasema Kateryna. “Baadhi yao walifariki vitani muda mfupi baadaye, na wengine walikufa katika mazingira ya kutatanisha.”
“Serikali ilimchukua mwanangu na kumpeleka vitani, na kuurejesha mwili wake kwaenye mfuko wa kubeba maiti. Yaliishia hapo. Hakuna usaidizi, hakuna ukweli, yani hakuna chochote kinachofanyika.
Chanzo cha picha, Reuters
Hadithi ya Mariyana kutoka Kyiv, pia ni ya kuvunja moyo vivyo hivyo. Yeye pia ameomba utambulisho wake na wa marehemu mume wake kutofichuliwa.
Mume wake Anatoliy alijitolea kupigana mwaka wa 2022. Hapo awali alikataliwa kwa sababu ya kutokuwa na uzoefu wa kijeshi lakini “aliendelea kurudi hadi walipomchukua”, anasema huku akitabasamu.
Anatoliy alitumwa kama mpiga risasi-za rasharasha karibu na Bakhmut, moja ya vita vya umwagaji damu zaidi.
“Alisema kwamba, baada ya operesheni moja, watu wapatao 50 waliuawa,” Maryana anakumbuka. “Alirudi akiwa tofauti; mtulivu; mawazo yakiwa mbali.”
Baada ya kupoteza sehemu ya mkono wake, Anatoliy alipelekwa hospitalini. Joni moja baada ya kupelekwa hospitali na na mke wake, alijitoa uhai.
“Vita ilimvunja,” anasema huku akitokwa na machozi. “Hakuweza kuishi na kile alichokiona.”
Kwa sababu Anatoliy alikufa kwa kujiua, hakufanyiwa maziko kijeshi.
“Aliposimama kwenye mstari wa mbele, alikuwa na manufaa. Lakini sasa yeye si shujaa?”
Mariyana anahisi kusalitiwa: “Hali iliniumiza sana. Niliwakabidhi mume wangu, na wakaniacha peke yangu bila chochote.”
Pia amehisi unyanyapaa kutoka kwa wajane wengine.

Msaada pekee anaopata unatoka kwa kikundi kidogo cha wanawake wanaokabiliwa na hali kama yake mtandaoni – wajane wa wanajeshi waliojitoa uhai.
Wanataka serikali ibadilishe sheria, ili familia zilizofiwa ziwe na haki sawa na kutambuliwa.
Viktoria, ambaye tulikutana naye huko Lviv, pia hawezi kuzungumza hadharani kuhusu kifo cha mume wake kwa kuhofia kukosolewa.
Mumewe Andriy alikuwa na ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa, lakini alisisitiza kujiunga na jeshi. Alikua dereva katika kitengo cha upelelezi na alishuhudia baadhi ya vita vikali, ikiwa ni pamoja na ukombozi wa Kherson.
Mnamo Juni 2023, Viktoria alipigiwa simu na kufahamishw akuwa Andriy amejitoa uhai.
“Nilihisi kana kwamb ulimwengu umeanguka,” anasema.
Mwili wake ulirejeshwa nyumbani siku 10 baadaye, lakini aliambiwa hangeweza kuuona.
Wakili wake baadaye alibaini kitu kisichokuwa cha kawaida katika uchunguzi wa kifo chake. Picha kutoka eneo la tukio zilimfanya atilie shaka tchanzo rasmi ch a kifo cha mume wake. Jeshi la Ukraine limekubali kufungua tena uchunguzi huo, kwa kutambua kushindwa.
Sasa anapigania kufungua tena kesi: “Ninapigania jina lake. Hawezi kujitetea tena. Vita yangu haijaisha.”
