Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitizia kuendelea kwa ushirikiano wa kimkakati na ushirikiano kati ya Tehran na Moscow.
Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ameandika makala kwenye gazeti la Kommersant kwamb,a ushirikiano kati ya Tehran na Moscow ni ushirikiano wa kimkakati katika njia ya mfumo mpya wa pande nyingi.
Jumanne iliyopita (16 Desemba), Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mjini Moscow, alikutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya maafisa wa Bunge la nchi hiyo Duma na Baraza la Juu vikiwa vyombo viwili vya bunge la Rusia.
Kwa upande mwingine, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Naibu Waziri Mkuu wa Rusia walikutana mjini Tehran na kusisitiza umuhimu wa kuharakisha Korido ya Kimkakati ya Kaskazini-Kusini.
Vitaly Savelyev, Naibu Waziri Mkuu wa Russia, alikutana na kufanya mazungumzo na Ali Larijani katika Sekretarieti ya Baraza Kuu la Usalama la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; mkutano uliofanyika kwa minajili ya kuendeleza makubaliano ya ngazi ya juu kati ya marais wa Ruusia na Irana kwa lengo la kuondoa vikwazo vilivyopo na kuingia katika awamu ya utekelezaji.
Wakati wa mkutano huo mjini Tehran, pande hizo mbili zilichunguza Korido ya Kaskazini-Kusini kama kigezo muhimu katika siasa za kijiografia za eneo hilo. Larijani alisisitiza wakati wa mkutano huo: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanya uamuzi wake wa kuifanya korido hii ianze utekelezaji.”

Wakati wa mkutano huo, pande zote mbili zilisistiza kuwa Korido ya Kaskazini-Kusini ni sehemu ya mkakati wa pamoja wa Iran na Russia wa kuanzisha ushirikiano endelevu na kubainisha njia huru za kikanda.
Duru mpya wa mazungumzo na mikutano kati ya maafisa wakuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia mjini Tehran na Moscow, inaashiria kuwa maafisa wakuu wa nchi hizo mbili wanakusudia kuimarisha ushirikiano wao katika nyanja za kisiasa, kiusalama, na kiuchumi.
Ushirikiano wa kimkakati kati ya Iran na Ruussia, ukiwa na mkazo wake kwenye Korido ya Kaskazini-Kusini, unaonyesha kuwa uhusiano wa nchi hizo mbili umeenda mbali zaidi ya ushirikiano wa muda na kuwa mkakati wa muda mrefu na endelevu. Ushirikiano huu unafungua njia ya kupunguza utegemezi kwa sarafu ya dola, kukabiliaa na vikwazo vya Marekani, na kupanua biashara na uwekezaji wa pamoja.
Katika uga wa jiopoliki, Korido ya Kaskazini-Kusini, ikiwa njia ya kimkakati, inaimarisha nafasi ya Iran kama kitovu cha usafirishaji cha kanda, inaiwezesha Russia kuwa na njia mbadala na salama ya biashara ya kimataifa, na inapelekea ukuaji wa korido za kikanda na kupungua kwa utegemezi wa njia zilizowekwa na nchi za Magharibi.
Katika nyanja za kisiasa na usalama, Iran na Russia, kupitia ushiriki wao hai katika BRICS na Jumuiya ya Ushirikiano la Shanghai, zina nafasi muhimu katika kuunda mfumo mpya wa pande nyingi na kukabiliana na mashinikizo ya Magharibi.

Katika ngazi ya juu kabisa ya kufanya maamuzi, juhudi endelevu za maafisa wa nchi zote mbili za kuondoa vikwazo na kuifanya korido hiyo iweze kufanya kazi zinaonyesha dhamira ya dhati ya kuanzisha ushirikiano wa kudumu na wa kimkakati. Ushirikiano kati ya Iran na Russia si ushirikiano wa pande mbili tu bali ni sehemu ya mkakati mpana zaidi wa kikanda na kimataifa ambao unaweza kuunda mustakabali wa utaratibu mpya wa pande nyingi na uhuru wa njia za kiuchumi na kisiasa za Eurasia.
Mkataba wa Kimkakati wa Kina kati ya Iran na Rusia uliosainiwa mjini Moscow mwaka 2024 kati ya Rais wa wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ebrahim Raisi na Rais Vladimir Putin wa Russia, ulikuwa hatua muhimu katika kupanua uhusiano kati ya Tehran na Moscow.
Mkataba huu ni ramani ya njia ya kimkakati kwa mustakabali wa uhusiano wa nchi hizo mbili, ambao sio tu unasaidia kukabiliana na vikwazo na mashinikizo ya Magharibi, bali pia unaimarisha nafasi ya Iran na Rusia katika mfumo mpya wa kimataifa wa kambi kadhaa na unawezesha njia za kikanda huru kama vile Korido ya Kaskazini-Kusini.