Karibu wakulima 7,300 wa Ulaya wameandamana kupinga makubaliano ya EU-Mercosur huko Brussels siku ya Alhamisi, Desemba 18. Maandamano hayo yaliandaliwa siku ambayo wakuu wa nchi na serikali wa nchi 27 wanachama wa EU walikuwa wakikutana kwa mkutano wa kilele.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano yalitokea katika eneo la Ulaya la mji mkuu wa Ubelgiji. Vikosi vya usalama vilikomesha maandamano hayo. Jioni ya siku hiyo, Rais wa Tume ya Ulaya alitangaza kuahirishwa kwa kusainiwa kwa makubaliano ya EU-Mercosur hadi mwezi Januari, baada ya kushindwa kupata idhini ya idadi kubwa ya nchi wanachama inayohitajika huko Brussels siku ya Alhamisi.

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen aliwafahamisha viongozi wa nchi 27 wanachama wa EU, waliokutana huko Brussels, kuhusu kuahirishwa hadi mwezi Januari kwa kusainiwa kwa makubaliano ya biashara kati ya EU na nchi za Mercosur kulingana na vyanzo vya kidiplomasia.

Ursula von der Leyen alitarajia kuanzisha makubaliano haya ya biashara huria siku ya Jumamosi, katika mkutano wa kilele wa Mercosur katika jiji la Foz do IguaƧu nchini Brazil. Lakini alihitaji idhini ya awali ya idadi kubwa ya nchi wanachama inayohitajika huko Brussels, ambayo hakuipata, haswa kutokana na upinzani wa Ufaransa na Italia.

Maelfu ya wakulima waonyesha hasira zao

Waandamanaji wenye hasira waliwasha moto matairi yaliwashwa, na kurusha viazi na vilipuzi, huku polisi wakirusha maji na gesi ya machozi… Mapema siku hiyo, maelfu ya wakulima wa Ulaya walionyesha hasira zao huko Brussels siku ya Alhamisi, Desemba 18, dhidi ya makubaliano ya biashara yaliyopendekezwa na Mercosur.

Msafara wa wakulima wa Ulaya ulioanza kutoka kituo cha treni cha Gare du Nord saa sita mchana haukuendelea rasmi hadi Place du Luxembourg kama ilivyopangwa awali. Maandamano hayo yalisitishwa katika barabara ya ndani, kulingana na Gazeti la Le Soir. Mtu mmoja alijeruhiwa vibaya pembezoni mwa maandamano.

Idadi mkubwa ya polisi ilitumwa kulinda taasisi za Ulaya, katikati ya mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi na serikali wa EU, ambao ulifunguliwa siku ya Alhamisi huko Brussels. Hali ilikuwa ya wasiwasi hasa katika Place du Luxembourg, mbele ya Bunge la Ulaya, shirika la habari la AFP limeripoti.

Kulingana na hesabu iliyotolewa na polisi wa Brussels, watu 7,300 walishiriki katika maandamano yaliyoidhinishwa, ambayo yalipitia mji mkuu wa Ubelgiji, yakiambatana na matrekta takriban hamsini, na kwa kiasi kikubwa yalikuwa ya amani. Zaidi ya hayo, matrekta 950, kulingana na chanzo hicho hicho, yalikuwa yamekusanyika katika eneo la  Ulaya, yakizuia mitaa kadhaa.

Kuanzia asubuhi na mapema, polisi walitumia mizinga ya maji kuwatawanya baadhi ya waandamanaji, na moto uliohusisha matairi na makopo ya taka uliziba maandamano hayo, na kutoa moshi mwingi mweusi. Watu waliovaa barakoa walivunja madirisha kadhaa ya jengo la Bunge, mwandishi wa habari wa AFP alishuhudia.

Makubaliano ya Mercosur, ushuru wa mbolea, mageuzi ya Sera ya Kilimo ya Pamoja (CAP): malalamiko ni mengi, waandamanaji kadhaa walisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *