Waziri Wa Uchukuzi Prof Makame Mbarawa Amesema Serikali Itaendelea Kukiwezesha Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji NIT Ili Kusaidia Katika kafanya tafiti na Kuzalisha Wataalamu Wenye Weledi Watakaotatua Changamoto Mbalimbali Zinazoikabili Sekta Ya Usafirishaji Nchini.
Akizungumza katika Mahafali ya 41 ya NIT yaliyofanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa chuo hicho Waziri wa Uchukuzi, Profesa Mbarawa amesema ongezeko la idadi ya wahitimu katika maeneo ya kimkakati ikiwemo usafiri wa anga, reli na majini linaendana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika miundombinu ya usafiri, jambo linaloongeza mahitaji ya rasilimali watu wenye ujuzi wa hali ya juu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la NIT, Profesa Ulingeta Mbamba, alisema chuo kitaendelea kuboresha ubora wa mafunzo kwa kuimarisha rasilimali watu na mifumo ya ufundishaji, kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kukuza uchumi shindani na endelevu.