Waziri Albanese ameitoa kauli hiyo Jumamosi, baada ya kuhudhuria ibada katika sinagogi mjini Sydney kwa ajili ya maombolezo ya waathiriwa wa shambulio la risasi lililotokea wakati wa sherehe ya Hanukkah kwenye ufukwe wa Bondi Jumapili iliyopita.

Tukio hilo la Bondi   lililosababisha vifo vya watu 15, ni baya zaidi nchini Australia kwa karibu miongo mitatu na sasa linachunguzwa kama kitendo cha ugaidi dhidi ya Wayahudi. Mamlaka za Australia zimeimarisha ulinzi kote nchini humo na kuweka sheria kali zaidi za umiliki wa bunduki ili kuzuia vitendo kama hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *