
Azimio hilo lilipigiwa kura Ijumaa na kikosi hicho kimeongezewa muda wa mwaka mmoja wa ziada hadi Disemba 20, 2026 huku Marekani ikitoa wito kwa vikosi vya Rwanda na waasi M23 kuheshimu makubaliano ya amani ya kikanda kufuatia vurugu zinazoendelea kushuhudiwa mashariki mwa DRC.
Mwakilishi wa Marekani katika mkutano huo Jennifer Locetta, amesema “mazungumzo ya kuiongezea muda MONUSCO yalitiwa kiwingu na mwenendo wa Rwanda na waasi wa M23 wa kuhujumu mchakato thabiti wa amani.”
Kikosi cha MONUSCO chenye wanajeshi 11,500 ni moja ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vinavyoungwa mkono na Marekani. Lakini utawala wa rais Donald Trump ulijaribu kupunguza mchango wake wa kifedha kwa Umoja wa Mataifa hasa katika eneo la ulinzi wa amani duniani.