WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amekagua maendeleo ya ujenzi wa madaraja na ukarabati wa barabara kuu ya Marendego-Nangurukuru-Lindi-Mingoyo.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Dk Mwigulu amewaambia wakazi wa Somanga mkoani Lindi kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anatekeleza miradi ya kimkakati ili kushughulika kwa vitendo na umasikini wa Watanzania.

Amesema kuwa Rais Samia amesimamia ukamilishaji wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere ili kuhakikisha kila mtanzania ananufaika na huduma ya nishati ya umeme.

“Tumeshuhudia Rais Dk Samia namna anavyotekeleza miradi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo uvuvi, maji, kilimo, afya, elimu na hata uwezeshaji wananchi kiuchumi,” amesema.