#HABARI: Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam imefanya mafunzo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana, Watu wenye ulemavu na wazee kuhusu ”Sheria ya Ununuzi wa Umma” na kutoa uelewa juu ya matumizi ya mfumo wa ununuzi (NeST) na fursa za asilimia thelathini ya bajeti ya ununuzi wa umma kwa makundi maalum.
Mafunzo hayo yamefanyika Katika ukumbi wa Karemjee jijini Dar es salaam, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa PPRA amewakilishwa na Bw. Hussein Jumanne, huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mh. Edward Mpogolo akiambatana na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndugu Elihuruma Mabelya.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.