Bodi ya utendaji ya Shirika la Fedha la Kimataifa siku ya Ijumaa, Desemba 19, imeidhinisha kitita kingine cha dola milioni 445 kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo ya fedha ya kimataifa ilmebainisha kuendelea kwa programu mbili zinazoendelea za ufadhili na nchi hiyo. Uamuzi huu unaruhusu ugawaji wa haraka wa dola milioni 445, na kufanya jumla ya kiasi ambacho tayari kimetolewa kufikia takriban dola milioni 785.

IMF inabainisha kwamba karibu ahadi zote zimetimizwa na mamlaka ya Kongo. Hata hivyo, inahimiza serikali kuendelea na mageuzi, kudumisha nidhamu kali ya fedha, na kulinda matumizi ya kijamii.

Habari zaidi zinakujia…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *