Kampeni za kugombea ubunge jimbo la Siha zinaendelea huku Chama cha Mapunduzi CCM kikiweka bayana dhamira ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yale aliyoahidi kuyatekeleza ndani ya siku 100 yalifanyiwa kazi ikiwemo mpango wa bima ya afya kwa wote akianza na makundi maalum Watoto,wajawazito na wazee huku kikiwataka vijana kuilindi amani ya taifa hili na kutokubali kutumika na wasioitakia nchi hii mema.
Kauli hiyo imetolewa na mbunge Viti Maalum mkoa wa Arusha Cecilia Parreso akinadi Ilani ya CCM pamoja na kuwaeleza wananchi kuwa kufuatua serikali kutambua umuhimu wa vijana Mhe Rais ameunda Wizara yao ili kutambua mahitaji yao na kuyafanyia kazi.
Mhe.Paresso amesema uchumi wa kanda ya kaskazini unategemea sekta utalii ambayo kwa sasa imeendelea kuimarishwa na kuvutia watalii wengi zaidi.
Uchaguzi wa mbunge katika jimbo unatarajiwa kufanyika desemba 30 mwaka huu na kwa upande wa CCM Dkt.Godwin Molle l amepewa ridhaa ya kupeperusha Bendera ya chama hicho.
#kilichoborakabisa