
Katika muda wa siku mbili zilizopita, boti za doria za walinzi wa pwani wa Ugiriki na zile za shirika la ulinzi wa mipaka barani Ulaya (Frontex), zimewaokoa baharini wahamiaji zaidi ya 650.
Watu hao walipekwa kwenye kambi mbalimbali za wakimbizi kisiwani humo. Hali ya hewa tulivu iliyoshudiwa eneo hilo imepelekea wasafirishaji haramu kutuma boti zaidi kuelekea barani Ulaya, huku idadi kubwa ya boti hizo zikitokea kwenye bandari ya Libya ya Tobruk.
Mwaka huu pekee, kisiwa cha Crete kimewapokea takriban wahamiaji 18,000 ikilinganishwa na 5,000 mwaka jana. Safari hizo za kutumia mashua ni hatari mno. Karibu wiki mbili zilizopita, makumi ya watu walikufa maji kusini mwa Crete baada ya boti yao kuzama.