#MICHEZO:Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, amesema Kikosi Cha timu ya Tanzania Taifa Stars, haikuvaa vazi lenye utambulisho wa Taifa wakati ikiwasili Morocco kwenye mashindano ya AFCON kutokana na Tanzania kutokuwa na vazi rasmi la Taifa.

Ndimbo amesema baadhi ya mashabiki walitarajia kuwaona Stars wakiwa na vazi la Kimaasai, huku wengine wakitumia teknolojia kuongeza picha zinazoonyesha wakiwa wamevaa vazi la kabila hilo, na kwamba vazi la Kimaasai haliwezi kuwakilisha rasmi Tanzania kwani kabila hilo linapatikana nchini Kenya.

Kadhalika Ndimbo, amesema Timu ya Taifa ya Taifa Stars, imepiga hatua katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), kwa kushiriki kwa mara ya nne na ikiwa ni mara ya tatu mfululizo hatua iliyochukua miaka mingi kufikiwa, hivyo shauku kubwa ya Watanzania ni kuona Taifa Stars ikipiga hatua zaidi katika mashindano hayo.

Aidha amewataka kujipongeza hata kwa mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa kwani imechukua muda mrefu kwa timu hiyo kurejea AFCON baada ya kushiriki mara ya mwisho mwaka 1980, kabla ya kurejea tena mwaka 2019, 2023 na wakati huu 2025.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *