Dar es Salaam. Gen Z wana mkwara sana. Sanaa! Mkwara ambao hata wao hawajui ni mkwara wa nini. Ila wameamua kujijaza na kupiga mkwara mzito. Big Man Majizzo kajaa kwenye 18 yao vizuri tu. Mkwara ukamtoa nje ya chaki. 

Ni Gen Z ambao kila kitu kwao ni mtandaoni. Kuanzia kuvaa, kula, kutongoza, kupiga stori, kusali nk. Ndo hao wanapost kitu na kisha wanakupiga mkwara, eti usipite hapa bila kukomeni neno ameni. 

Wanaandika xaxa badala ya sasa. Hawaeleweki wanafupisha neno au wanarefusha. Hao hao ambao huandika ‘jamani nataka laiki 100 kwenye komenti yangu”, nao Gen Z wenzake kweli wana ‘laiki’. 

Hizi njegere ambazo hulala muda wote geto na mabando. Zinaanza kumtusi Wema kwa kutokuwa na mtoto. Wanajua kutumia simu na kunywa pombe kuliko usafi wa maeneo nyeti ya miili yao. 

Wanajua majina ya pombe, viatu na mistari ya singeli, kuliko jina la ukoo wao. Wengi wamezaliwa, wamesoma, kukulia, kuoa/olewa au kuzalishwa kwenye kata hiyo hiyo. Upeo na tafakari sifuri.

Kizazi cha milenia kilikuwa na hofu sana. Kwamba nikifanya hili mama yangu atakuwa kwenye hali gani? Nikifanya hivi familia itanielewaje? Lakini hawa Gen Z hawana hofu hiyo kabisa.

Wanakuaje na hofu na wao kwao wanamjua mama tu? Nje yake labda bibi ama mjomba tu. Tena mjomba mwenyewe siyo toka nitoke ni mama. Ni kibwana cha mamaake ndo anakiita Anko.

Kitoto kimezaliwa kwenye taksi  kona ya Fire. Mamtu akikimbizwa muhimbili, uchungu kapatia bar akilewa. Mimba yake ilitungiwa guest akiwa njwii, hamkumbuki bwana mwenyewe.

Mtoto anazaliwa anafahamiana na wauza urembo. Mashangazi wa mtaani wenye ushostito na mama. Bodaboda wanaombeba mama ulevini na wale maanko wanaokuja mara kwa mara usiku.

Mama mwenyewe alikuja mjini miaka mingi nyuma. Hajawahi kurudi kwao Singida kama siyo Babati. Na yeye aliletwa na dada kwa gia ya kuja kufanya kazi za salon kama siyo kushona. 

Watoto wengi wa sasa ni uzao wa ‘singo maza’. Ikiwepo vifo vingi vya wanaume, kukimbia jukumu au kuzaa na waume za watu. Ndo maisha ya sasa, kwani wengi wao huona bora kuzaa kuliko ndoa.

Ndo watoto waliojazana mijini kwa sasa. Ajira kubwa bodaboda, kubet, winga, udalali wa vitu au watu. Pesa za mitandaoni kama ‘tikitoku’, yutyubu, umarioo na udananda mwingi mjini.

Uchawa ni mchongo kwa sasa. Kuna uchawa kwa matajiri na kuna uchawa kwa wanawake wenye utamanishi. Yaani dem mwenye kuhusudiwa na wengi watu hujiweka pembeni. 

Yaani dem akiwa na mtoko na bwana naye yupo pembeni. Kazi yake kubeba vipochi, kubeba simu na kupokea ili dem asigonganishe ndinga. Yaani wakati anatumikia penzi la bosi mpya asihofu. 

Akitoka kusulubiwa anaenda kulewa na kula bata na chawa wake. Yaani kuna wababa mjini wanahudumia mwanamke na mpambe wake wa kiume ambaye naye ana familia. 

Yaani baba wa watu anahudumia familia yake, nyumba ndogo na chawa wake mwenye familia ya mke na watoto kadhaa. Huduma zinaenda ‘dairekti au indairekti’ kutegemea na pesa danga. 

Haya ndo maisha ya Gen Z wenu hawa wanaowapiga mkwara. Hizi ngisi za kuitwa Gen Z haziwezi na hazijwahi kumiliki akili timamu. Ni kama AI za mitaani zenye damu na mifupa. Kuna kazi.
Hawa Gen Z hawajawahi kucheza komborela wala mdako.

Hawajui marede wala ukuti ukuti. Wanajua kulaiki, kukomenti na kushea ama kutukana watu mitandaoni. Siyo wabunifu kwanza.

Matusi mengi ukisoma hakuna tusi jipya, ni matusi tuliyoyabuni kizazi cha milenia. Bahati mbaya matusi yetu ya mdomoni kwao  huyafanya mwilini kweli kweli. Ni hilo tu ndo jipya. 

Hatuwezi kupigwa mikwara na hawa Gen Z aiseee. Wanatakiwa kukaa chini na kusoma michezo iliyochezwa kabla katika nyakati zetu. Uzuri Milenia na Gen Z kuna kauhusiano kiasi. 

Hizi stori za kugomea kazi ama nyimbo za wasanii ni mikwara kama mikwara mingine. Hawa milango ya gereza ilifunguka yenyewe nyakati zile za Paulo na Sila itakuwa sasa? 

Stori za kuomba msamaha weka pembeni. Mijadala na maongezi weka kando. Kamateni Diamond na Alikiba, waingize studio leo hii. Waambie wadondoshe pini moja la pamoja. 

Redio mbao zote zitazimwa na nchi nzima itaimba goma moja. Hakuna kuombana msamaha wala kusameheana. Weka dude juu ya dude kisha waache nchi nzima iimbe wimbo mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *