Shirika la Mabalozi wa Usalama Barabarani linalofanya shughuli zake ndani ya mikoa ya Tanzania Bara limewataka abiria wanaosafiri kuelekea mikoa mbalimbali nchini kupaza sauti kuhusu changamoto za usafiri zikiwemo kupandishiwa nauli, mabasi yasiyokidhi ubora, mwendo usioridhisha na unyanyasaji mwingine unaoweza kujitokeza safarini.
Shirika hilo limesema abiria wengi wamekuwa chanzo cha matatizo ya usafiri kutokana na kuogopa kueleza matatizo wanayokutana nayo na ndio maana Disemba hii limejikita katika kampeni ya ‘Usikubali Kupigwa’ ili kuwasaidia abiria hao.
Imeandaliwa na Robert Mayungu.
Mhariri @moseskwindi