Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza siku ya Ijumaa, Desemba 19, kwamba kundi la Islamic State lililengwa kwa mashambulizi ya “kulipiza kisasi kikali” nchini Syria. Angalau wanachama watano wa ISIS waliuawa katika mashambulizi ya anga ya Marekani. Hii inakuja baada ya shambulio karibu wiki moja mapema ambalo liliwaua wanajeshi wawili wa Marekani na mkalimani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Tunashambulia ngome za ISIS kwa nguvu sana,” ameandika Rais wa Marekani Donald Trump kwenye jukwaa lake la Truth Social, muda mfupi baada ya Pentagon kutangaza kuanza kwa operesheni “kubwa”. Jeshi la Marekani limeanza operesheni nchini Syria ili “kuwaangamiza wapiganaji wa Islamic State, miundombinu, na maeneo ya silaha,” mkuu wa Pentagon Pete Hegseth alitangaza kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Angalau wanachama watano wa kundi la Islamic State waliuawa katika mashambulizi haya ya anga ya Marekani, Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (SOHR) limeripoti leo Jumamosi. Miongoni mwao ni “kiongozi wa kundi hilo” anayehusika na masuala ya ndege zisizo na rubani katika eneo hilo, Rami Abdel Rahman, mkuu wa shirika hilo lisilo la kiserikali, ameliambia shirika la habari la AFP, akiongeza kuwa waliuawa katika mkoa wa mashariki wa Deir ez-Zor.

Hii ilikuwa “jibu la moja kwa moja” na “tamko la kulipiza kisasi” baada ya shambulio lililowaua wanajeshi wawili wa Marekani na mkalimani mmoja nchini Syria siku ya Jumamosi, Desemba 13, ameongeza, akisema: “Leo tumewasaka na kuwaua maadui. Maadui wengi. Na tutaendelea.”

Mashambulizi haya yanatumika kama ukumbusho kwamba, licha ya kuanguka kwa ukhalifa, Dola ya Kiislamu inabaki hai katika jangwa la Syria, ambapo Marekani ina wanajeshi wapatao 1,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *