Chanzo cha picha, Kobbie Mainoo
Muda wa kusoma: Dakika 3
Kiungo wa England Kobbie Mainoo, 20, haoni mustakabali wake Manchester United chini ya kocha Ruben Amorim na yuko tayari kuiacha kwa uhamisho wa kudumu klabu yake ya utotoni mwezi Januari. (Mail)
Vilabu vya Manchester United, Manchester City, Liverpool na Tottenham vimeanza mazungumzo na winga wa Ghana mwenye umri wa miaka 25 Antoine Semenyo kuhusu dili la pauni milioni 65, lakini vitalazimika kukamilisha makubaliano na Bournemouth kabla ya tarehe 10 Januari ili kumpata. (The i)
Manchester United wanaamini Semenyo anaweza kuimarisha upande wa kushoto, huku Amorim akiwa na mashaka juu ya mchezaji wa Denmark Patrick Dorgu, 21, aliyesajiliwa kwa pauni milioni 25 mwezi Februari kutoka Lecce. (Sun)
Bournemouth wanamwona winga wa Tottenham na Wales Brennan Johnson, 24, kama mbadala iwapo Semenyo ataondoka. (Teamtalk)
Chanzo cha picha, Getty Images
Hata hivyo, Bournemouth huenda wakakutana na ushindani kutoka Crystal Palace, ambao pia wameonyesha nia ya kumsajili Johnson kutoka Spurs. (Guardian)
Barcelona wanaonekana kuwa karibu zaidi kukubali kipengele cha kulipa pauni milioni 26 ili kumsajili Marcus Rashford kutoka Manchester United, huku mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 28 akirejea katika kiwango bora akiwa kwa mkopo Hispania. (Mundo Deportivo)
Mshambuliaji wa Kifaransa wa Sassuolo mwenye umri wa miaka 27 Armand Lauriente anatarajiwa kulazimisha uhamisho wa Januari kutokana na tetesi zinazoendelea zinazomuhusisha na klabu ya Sunderland. (Sunderland Echo)
Real Madrid wamejitokeza kama moja ya timu zinazoweza kumsajili kiungo wa Al-Hilal na Ureno Ruben Neves, 28, mwezi Januari. (Fichajes)
Chanzo cha picha, Getty Images
AC Milan wanataka beki wa Brazil Thiago Silva, 41, kurejea klabuni wakati wa dirisha la usajili wa majira ya baridi baada ya kuvunja mkataba wake na Fluminense kwa makubaliano ya pande zote. (ESPN)
Nahodha wa Brighton Lewis Dunk, 34, ameongeza mkataba wake kwa mwaka mmoja kutokana na idadi ya mechi alizocheza, na sasa atabaki klabuni hapo hadi 2027. (Sky Sports)
Manchester United, Newcastle na Aston Villa zote zina nia ya kumsajili winga wa Inter Milan na Uholanzi Denzel Dumfries, 29. (Teamtalk)
Barcelona inatarajiwa kukamilisha mpango wa kushtua wa kusajili nyota mwenye kipaji kutoka Norwich mwenye umri wa miaka 15 Ajay Tavares, ambaye tayari ameichezea timu ya taifa ya England chini ya miaka 17. (Sun)
Aliyekuwa kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane, kocha wa Strasbourg Liam Rosenior, na kocha wa Como Cesc Fabregas ni miongoni mwa majina yanayofuatiliwa na Chelsea iwapo kocha wa sasa Enzo Maresca ataondoka Stamford Bridge. (Caught Offside)