Wito wa Baraza hilo umetolewa wakati mapigano katika eneo hilo lenye utajiri wa madini yakiongezeka licha ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Marekani.

Chombo hicho chenye nguvu zaidi cha Umoja wa Mataifa kimelaani shambulio la hivi karibuni la waasi wa M23 huko Uvira, na kuitaka Rwanda kuacha kuwaunga mkono waasi hao na kuwaondoa wanajeshi wake katika ardhi ya Kongo. Aidha, Baraza hilo limeidhinisha azimio la kurefusha muda wa mwaka mmoja hadi Desemba 2026 wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo, MONUSCO.

Kikosi hicho chenye askari karibu 12,000, kilitumwa kwa mara ya kwanza nchini Kongo mwaka 2010, lakini miaka 15 baadaye, Wakongomani wengi wanasema  MONUSCO haikutoa ulinzi unaohitajika  na raia wakati wa mashambulizi ya makundi ya waasi, na mara kadhaa kumefanyika maandamano ya kukipinga kikosi hicho chenye jukumu kubwa zaidi la kuwalinda raia na usambazaji wa misaada ya kibinaadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *