Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kwa kauli moja sikuya Ijumaa kuongeza muda wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mwaka mwingine mmoja, ambapo mvutano unaendelea mashariki mwa nchi. Azimio hilo linaongeza muda wa “hadi Desemba 20, 2026, kwa MONUSCO nchini DRC,” ambayo ina takriban wanajeshi wa kulinda amani 11,500 nchini humo.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kwa kauli moja siku ya Ijumaa, Desemba 19, kuongeza muda wa kikosi chake cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) kwa mwaka mwingine mmoja, ambapo mvutano unaendelea mashariki mwa nchi licha ya makubaliano ya amani kusainiwa jijini Washington, nchini Marekani.

Hii ni mojawapo ya misheni chache za Umoja wa Mataifa zinazoungwa mkono na Marekani chini ya utawala wa Donald Trump, ambayo inatafuta kutekeleza makubaliano ya amani ambayo ilisaidia kuratibu. Idadi ya walinda amani waliotumwa, takriban 11,500, bado haijabadilika, baada ya kupungua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni.

Kuimarisha jukumu la kisiasa la MONUSCO

MONUSCO inadumisha mamlaka yake ya mashambulizi, ikiwa na mamlaka ya kufanya operesheni zinazolenga makundi yenye silaha yanayoendesha harakati zao mashariki mwa nchi. Lakini azimio hilo linaimarisha jukumu lake la kisiasa.

Baraza la Usalama linatoa wito kwa ujumbe huo kuchukua jukumu kubwa katika kufuatilia na kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa huko Doha mnamo mwezi Oktoba, ambayo hayajatekelezwa. MONUSCO pia inaombwa kuzingatia maeneo yenye mvutano Kaskazini na Kusini mwa Kivu. Hili ni jambo muhimu kwa sababu, linafungua njia ya uwezekano wa kurudi kwa MONUSCO Kusini mwa mkoa wa Kivu Kusini, ambapo ilijiondoa, ikiwa hali na rasilimali zinaruhusu.

Azimio hilo pia lina jukumu la kuunga mkono mamlaka ya Kongo katika kupokonya silaha FDLR, kulingana na ahadi zao na mchakato unaoendelea wa amani.

Hatimaye, azimio lililopitishwa siku ya Ijumaa linathibitisha wazi masharti ya Azimio 2773 la mwezi wa Februari 2025, ambalo Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa Jeshi la Ulinzi la Rwanda kusitisha usaidizi wowote kwa M23 na kujiondoa kutoka ardhi ya Kongo. Marekani imebainisha msimamo wake: AFC/M23 lazima ijiondoe hadi takriban kilomita 75 kutoka Uvira, katika mkoa wa Kivu Kusini, ambao iliuliteka wiki iliyopita, hadi Kamanyola, ngome yake ya awali.

Ahadi ya M23 ya kujiondoa kutoka mji wa Uvira haitoshi. M23 lazima ijiondoe mara moja hadi angalau kilomita 75 kutoka Uvira na kuzingatia majukumu yake yote chini ya makubaliano ya mfumo. Tunalaani vikali hatua ya M23 kuingia Uvira na kwingineko, pamoja na uungaji mkono wa Rwanda kwa M23, kinyume na majukumu yake chini ya Makubaliano ya Washington. Marekani   inaendelea kujitolea sana kwa makubaliano ya Washington na ahadi zake za amani na ustawi kwa mashariki mwa DRC na kuunga mkono juhudi ndani ya mchakato wa Doha. Tunategemea heshima kamili ya pande zote mbili kwa makubaliano yote mawili. Ikiwa M23 na Rwanda watachagua kuheshimu ahadi zao, MONUSCO, kupitia agizo hili, itaweza kusaidia utekelezaji wa michakato yote miwili.

Vikwazo hivi vimekwamisha kazi ya MONUSCO katika miezi ya hivi karibuni

Mamlaka ya sasa ya MONUSCO inamalizika leo Jumamosi, Desemba 20. Azimio la awali la Umoja wa Mataifa kuhusu misheni hii, 2765, liliidhinisha kikomo cha takriban wafanyakazi 13,800 (jeshi, polisi, na waangalizi). Vipaumbele vyake vya kimkakati vililenga ulinzi wa raia, usaidizi kwa utulivu na uimarishaji wa taasisi za serikali, pamoja na usaidizi wa mageuzi ya utawala na usalama. Licha ya mamlaka hii, inayochukuliwa kuwa imara, MONUSCO haijazuia kusonga mbele kwa AFC/M23 mashariki mwa nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *