Basi la abiria lililengwa huku malori yakiwaka moto katika eneo la maegesho ya magari. Taarifa hiyo iliyotolewa na Huduma ya Ulinzi wa Raia ya Ukraine haikuweza kuthibitishwa na vyanzo huru vya habari. Pia, jeshi la Ukraine limesema limeshambulia kwa droni na kuharibu kituo cha kuchimba mafuta cha “Lukoil” pamoja na meli ya kivita ya Urusi ya “Ochotnik” katika Bahari ya Caspian, takriban kilometa 1,800 kutoka pwani ya Ukraine.

Hayo yakiarifiwa, Mjumbe wa Urusi Kirill Dmitriev amesema hivi leo kuwa anaelekea katika mji wa Miami ambako duru nyingine ya mazungumzo ya kujaribu kuutatua mzozo wa Ukraine imepangwa kufanyika. Marekani imekuwa ikijaribu kwa muda sasa kuutafutia suluhu  mzozo huo  uliodumu kwa karibu miaka minne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *