Ziara ya Idris inalenga pia kujadili namna ya kuwezesha usambazaji wa misaada ya kibinadamu na uwezekano wa kufikiwa kwa mpango wa kusitisha mapigano. Hayo yameelezwa na vyanzo viwili vya serikali ya  Sudan  wakati mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF yakiendelea na kushika kasi katika jimbo la Kordofan, na hivyo kuzusha hofu ya kutokea ukatili mwengine kama ulioshuhudiwa katika mji wa El-Fasher mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Mapema mwezi huu, Guterres alisema kuwa Umoja wa Mataifa ulikuwa ukiandaa mazungumzo na pande zote mbili mjini Geneva, bila hata hivyo kutoa tarehe rasmi. Matumaini mapya ya kuutatua mzozo huo kwa njia za kidiplomasia yaliibuka mwezi uliopita wakati Rais wa Marekani Donald Trump alipoahidi kuwa ataingilia kati kujaribu kupatikana kwa suluhu, baada ya kuombwa kufanya hivyo na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *