#HABARI: Abiria waliokuwa wakisafiri kwa basi la Kampuni ya Super Zambia kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma wamenusurika kifo baada ya basi hilo kugongwa pembeni na lori la mafuta katika eneo la Mikese, Barabara Kuu ya Morogoro – Dar es Salaam.

Mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo Ngwenje Mohamed wamesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 9 usiku baada ya dereva wa lori la mafuta kujaribu kulipita basi hilo, hali iliyosababisha taharuki na baadhi ya abiria kupata mshtuko na majeraha madogo madogo.

ITV imetembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo madaktari walieleza kuwa hawajapokea majeruhi wa ajali hiyo, huku wananchi wakitoa tahadhari kwa madereva kuwa makini zaidi barabarani hasa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu na mwishoni mwa mwaka ambapo magari huwa mengi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *