#HABARI: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Serikali itaendelea kuthamini sauti za viongozi wa kiroho na kidini kama washirika muhimu katika ujenzi wa taifa lenye kuthamini haki na amani na usalama katika nchi huku akiwataka watanzania wawe wavumilivu na Serikali iko tayari kusikiliza na kujifunza ili taifa liendelee kuwa na amani umoja na mshikamano.

Ametoa kauli hiyo leo wilayani Karagwe mkoani Kagera wakati wa ibada ya Ubarikio wa Uchungaji ambapo jumla ya Mashemasi watano wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania wamebarikiwa kuingia katika Huduma ya Kichungaji huku Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Karagwe, Askofu Dkt.Benson Bagonza akisisitiza misingi mitano ya maridhiano baada ya matukio yaliyotokea Oktoba 29, mwaka huu.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *