Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limeendelea kutoa elimu kwa madereva na abiria pamoja na kufanya ukaguzi wa mabasi ya abiria, kama sehemu ya jitihada za kudhibiti ajali na kuimarisha usalama barabarani.

Zoezi hilo, lililoongozwa na Mkuu wa Operesheni wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Joseph Mwakabonga, limefanyika usiku wa kuamkia Disemba 21, 2025, katika eneo la Kikatiti mkoani Arusha, barabara kuu ya Moshi–Arusha.

Katika operesheni hiyo, baadhi ya mabasi yalibainika kufanya makosa ikiwemo kuzidisha abiria na mwendokasi, ambapo hatua za kisheria zilichukuliwa, huku akiwataka madereva kuzingatia kikamilifu sheria za usalama barabarani.

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *