
Mwakilishi wa kudumu wa Venezuela katika Umoja wa Mataifa amelaani madai ya Rais Donald Trump kwamba Marekani inamiliki eneo la nchi hiyo na rasilimali za mafuta, akionya kwamba enzi ya ukoloni wa kale imekwisha.
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wakati wa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ukoloni uligeuka na kawa eneo la kufichuliwa waziwazi sera za Ikulu ya White House. Samuel Moncada, Mwakilishi wa Kudumu wa Venezuela katika Umoja wa Mataifa, alielezea kauli za hivi karibuni za Rais wa Marekani, ambaye alikuwa ametaka kusalimisha rasilimali za mafuta za Venezuela mara moja, kama tusi la kutisha na ukiukaji wa kanuni zote za ustaarabu wa binadamu.
Alisema kwamba Trump anakusudia kurudisha nyuma saa ya historia na kuirudisha Venezuela kuwa koloni.
Aidha balozi na mwakilishi huyo wa kuduma wa Venezuela katika Umoja wa Mataifa amesema: “Hakuna chombo cha kisheria duniani kinachoweza kukaa kimya mbele ya kauli hii mbaya. Ukoloni ni uhalifu wa kivamizi na utawala wa Trump unatwisha machafuko na uharibifu katika uhusiano wa kimataifa.”