Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, amewatolea mwito viongozi wa Umoja wa Ulaya kuonesha ujasiri na kusaini mkataba wa kibiashara na jumuiya ya kanda ya Amerika ya Kusini ya Mercosur .

EU, Mercosur kuunda kanda kubwa zaidi ya biashara duniani

Mataifa wanachama wa jumuiya hiyo, Argentina, Brazil Paraguay na Uruguay pamoja na mkuu wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen na mataifa mengi wanachama wa Umoja wa Ulaya, walikuwa na matumaini kwamba mkataba huo ungesainiwa jana Jumamosi na Umoja wa Ulaya ili kutoa fursa ya kuanzishwa soko huria kubwa zaidi duniani.

Hata hivyo mkataba huo umekabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wakulima hasa wa Ufaransa na Italia na sasa hatua ya kusaini imesogezwa hadi mwezi Januari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *