Mvua zilizoanza kunyesha katika Manispaa ya Tabora zimesababisha athari kwa baadhi ya makazi, ambapo nyumba kadhaa zimejaa maji katika Kata za Ali Hassan Mwinyi na Malolo, hali iliyosababisha malalamiko kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo.

Mbali na kuathiri makazi, mvua hizo zilizonyesha kuanzia asubuhi hadi mchana zimesababisha maji kufunika baadhi ya barabara za mitaani, hali iliyokatiza mawasiliano na kutishia usalama wa afya kwa wananchi kutokana na hatari ya magonjwa ya mlipuko.

Kufuatia hali hiyo, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, kupitia Meya wake Ghulam Dewij, imesema hatua za makusudi zinaendelea kuchukuliwa ili kukabiliana na adha hiyo na kupunguza madhara kwa wananchi waliokumbwa na changamoto hiyo.

✍Juma Kapipi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *