Msemaji wa ikulu ya Urusi Dmitry Peskov amekiambia kituo cha utangazaji cha serikali, Ria Novosti, kwamba rais Vladmir Putin yuko tayari kukaa mezani kwa mazungumzo na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.
Kwa mujibu wa Peskov, rais Putin anaamini mazungumzo na kiongozi huyo wa Ufaransa yanaweza kuwa na tija ikiwa itakuweko dhamira ya pamoja ya kisiasa.Volodymyr Zelenskiy
Ofisi ya rais Macron imesema imepokea tangazo hilo la Urusi na itachukua hatua ya kushughulikia kwa namna bora ndani ya siku chache zijazo.
Siku ya Ijumaa Macron alisema kwamba, litakuwa jambo muhimu kwa Ulaya na Ukraine kuzungumza na rais Vladmir Putin kwa mara nyingine, ili kuhusika moja kwa moja kwenye mazungumzo.Viongozi wa EU waafikiana kuufanyika kazi mpango wa kutumia mali za Urusi zilizozuiwa
Wakati huohuo taarifa zinasema, vikosi vya Urusi, vimevuka mpaka wa Ukraine kwenye mkoa wa Sumy na kuwateka wakaazi 50 wengi wakiwa ni wazee kutoka kijiji kimoja cha mpakani na kuwapeleka nchini Urusi.