Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa ameitaja hatua ya Misri ya kuidhinisha makubaliano ya ununuzi wa gesi kutoka kwa utawala wa Israel kuwa ni  uungaji mkono wa nchi hiyo kwa mauaji ya halaiki ya Wazayuni huko Gaza.

Francesca Albanese, Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa, huku akikosoa vikali makubaliano ya gesi kati ya Misri na utawala wa Israel, alisema kwamba makubaliano hayo yanaonyesha uungaji mkono wa Cairo kwa Tel Aviv katika mauaji ya halaiki ya Wapalestina.

Albanese aliongeza: “Misri inaweza kusema chochote inachotaka, lakini kununua gesi yenye thamani ya dola bilioni 35 kutoka kwa utawala wa Israel ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.” Alisisitiza kwamba makubaliano hayo ni ishara ya ajabu ya uungaji mkono kwa utawala wa Israel katika mauaji ya halaiki ya Wapalestina.

Kadhalika ametoa wito kwa nchi kutoweka kipaumbele maslahi ya kiuchumi kuliko maadili ya kibinadamu.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *