Shirika la Kitaaluma la Afrika la Utawala na Usimamizi wa Umma (AAPAM) limeitunuku tuzo Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ya ubunifu wa mifumo ya kidigitali kufuatia wasilisho la TFRA la utendaji kazi wa mfumo kidijitali wa pembejeo za ruzuku ambao umetajwa kusaidia kudhibti uuzwaji wa mbolea zilizo chini ya kiwango na kupatikana kwa takwimu sahihi za wakulima nchini.
Ushindi huo umeifanya Tanzania kung’ara ikifungana na Afrika Kusini.
Tuzo hiyo imetolewa katika Mkutano wa 44 wa Jumuiya ya Afrika ya Wataalam wa Usimamizi wa Utawala katika utumishi wa umma ulioshirikisha mamlaka 49.