Mapigano ya hivi karibuni ya eneo la mpakani kati ya mataifa hayo mawili, yamesababisha mauaji ya watu 22 nchini Thailand huku 19 wakiuwawa Cambodia. Maafisa wa pande zote mbili wanasema watu zaidi ya 900,000 wamelazimika kukosa makaazi kutokana na mzozo huo.

Malaysia ambayo ni mwenyekiti wa Jumuiya ya mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN, imesema inaamini mazungumzo ya Kuala Lumpur yatasaidia kufikiwa suluhu ya muda mrefu kati ya mataifa hayo. Akizungumza katika mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Malaysia, Mohamad Hasan amezihimiza pande hasimu na wawakilishi wa ASEAN kuupa umuhimu mkubwa mgogoro uliopo.

Taarifa zaidi zinasema Thailand na Cambodia tayari zimekubaliana kuwa na majadiliano zaidi ya kumaliza mzozo huo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand Sihasak Phuangketkeow amesema majadiliano hayo yatafanyika siku ya Jumatano Desemba 24, kama ilivyopendekezwa na Cambodia.

Cambodia na Thailand wamekubali kujadili mgogoro baina yao

Ameongeza kuwa tayari mkutano umepangwa kufanyika Disemba 24, kufuatia pendekezo la Cambodia.

Cambodia 2025 |
Maandamano ya kushinikiza Thailand na Cambodia kusitisha mapigano.Picha: Kim Jae-Hwan/SOPA Images/IMAGO

Lakini Waziri Sihasak ametahadharisha kuwa, mazungumzo hayo huenda yasitokea matokea  ya haraka, akisisitiza kuwa makubalino ya pande zote huenda yakachukua muda kufikiwa.

Mwishoni mwa mwezi Oktoba 2025, Thailand na Cambodia zilisaini makubaliano ya kusitisha mapigano katika hafla iliyohudhuriwa na Rais wa Marekani Donald Trump.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Thailand ilitakiwa kuwaachilia wafungwa wa Cambodia, huku Cambodia ikitakiwa nayo kuanza kuondoa silaha nzito katika maeneo ya mpakani.  

Lakini Siku chache baada ya utiaji saini huo, nchi hizo mbili zilianza tena kushambuliana huku zikiendelea kulaumiana kuhusu ukiukaji wa makubaliano hayo ya usitishaji vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *