Wizara ya Biashara ya China imetangaza leo kuwa huu ulikuwa uamuzi wa awali katika mwendelezo wa uchunguzi ulioanza Agosti 2024 na hatua hiyo itaanza kutekelezwa Disemba 23.

Viwango vya ushuru huo wa muda vilivyowekwa kwa sasa ni kati ya asilimia 21.9-42.7.

Brussels imeijibu hatua hiyo akisema haina msingi.

China inaishutumu Ulaya kwa kutoa ruzuku kubwa kwenye sekta yake ya maziwa, na kufanya uagizaji kutoka Ulaya kuwaathiri pakubwa wazalishaji wa China.

Mwaka 2023, Brussels nayo ilianzisha uchunguzi wa magari ya umeme yaliyotengenezwa China, ikiishutumu Beijing kwa kusaidia sekta hiyo kwa ruzuku kubwa za serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *