
Miaka mitatu baada ya kukamatwa kwake, Luteni Jenerali Philémon Yav Irung, aliyepewa jina la utani “Tiger wa Katangese” katika jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alikuwa akisikilizwa katika Mahakama Kuu ya Kijeshi huko Kinshasa tangu siku ya Ijumaa, Desemba 20.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Pascal Mulegwa
Kamanda huyo wa zamani wa kanda ya tatu ya Ulinzi—ambayo inaundwa mikoa saba kaskazini mashariki na mashariki mwa DRC—anashtakiwa, haswa kwa uhaini, kutokana na uhusiano anaoshtumiwa na Rwanda. Jenerali huyo anakabiliwa na adhabu ya kifo, ambayo hubadilishwa kimfumo kuwa kifungo cha maisha jela nchini DRC. Ndugu, jamaa na marafiki zake wanalaa shutma hiyo.
Kulingana na hati ya mashtaka iliyotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Majeshi ya Kongo nchini DRC, jenerali huyo mwenye nyota tatu anashtakiwa katika kesi mbili za uhaini, kushiriki katika uasi, na kuwashinikiza wanajeshi kufanya vitendo kinyume na wajibu au nidhamu.
Anashukiwa, haswa, kutenda vitendo vya uhaini kwa kudumisha uhusiano na Kigali. Miongoni mwa ushahidi dhidi yake ni kupemtumia Peter Cirimwami – ambaye wakati huo alikuwa kamanda wa operesheni dhidi ya AFC/M23 na aliyefariki Januari 2025 – ujumbe uliowasilishwa kama uliotoka kwa katibu wa Jenerali James Kabarebe, ambaye wakati huo alikuwa mshauri wa usalama wa Rais Paul Kagame. Katika ujumbe huu wa maandishi, Peter Cirimwami alishutumiwa kwa “kuchelewesha mradi wetu kwa uzito,” akimaanisha malengo ya Rwanda.
Wakati wa mkutano mwingine, katika hoteli ya Goma, Philémon Yav Irung inadaiwa pia alijaribu kumzuia afisa wa Kongo kujiunga na mapigano dhidi ya AFC/M23 au washirika wake katika mkoa wa Kivu Kusini.
Upande wa utetezi wa jenerali, ambao unadai bado haujapata hati zote kwenye faili la kesi, unafutilia mbali shutuma hizi, ambazo unaziona kuwa “hazina msingi.”
Masharti yake kabla ya kesi kuchunguzwa kuhusu uhalali wake na mkakati wake wa utetezi unatarajiwa kushughulikiwa katika kikao kijacho kilichopangwa kufanyika Januari 6, 2026.
Philémon Yav Irung alikuwa jenerali wa kwanza kukamatwa baada ya shambulio kubwa la waasi wa AFC/M23 katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Mfululizo huu wa mapigano ulisababisha waasi kuiteka Bunagana, kabla ya kutishia kuitea miji ya Goma na Bukavu, na kisha kusonga mbele, wiki mbili zilizopita, kuelekea Uvira.