#HABARI: Jeshi la Polisi Tanzania limethibitisha kuwa hali ya usalama nchini imeendelea kuwa shwari tangu kutolewa kwa ripoti ya usalama Desemba 12, 2025. Utulivu huo umechangiwa na ushirikiano wa Watanzania katika kulinda amani, hali inayowaruhusu wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku bila bughudha.

Katika kuelekea msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi limejipanga kuimarisha usalama wakati wote. Wananchi wamehimizwa kuthamini amani iliyopo na kukataa vitendo vyote vyenye lengo la kuvuruga utulivu wakati wa sherehe hizo na baada ya msimu wa sikukuu.

Aidha, jeshi limetoa rai kwa wasafiri kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika. Chini ya kauli mbiu ya “Endesha Salama, Familia Inakusubiri,” wananchi wameaswa kuwa waangalifu barabarani wanapoelekea kuungana na familia zao katika ibada na mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *