#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mheshimiwa Geofrey Timoth, ametembelea Kituo cha Polisi Salasala ambacho kilipata madhara kufuatia matukio ya Oktoba 29, na kuahidi atahakikisha kituo hicho kinarejea katika hali yake ya kawaida ili kiendelee kutoa huduma kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mh. Timoth amesema viongozi wana jukumu la kuyafanyia kazi yale yote yaliyoahidiwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hususan katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amesema utekelezaji wa Ilani unaendelea kuonekana katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Kawe ikiwemo kuanza kwa mipango ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara, akisisitiza kuwa hatua hizo si za bahati mbaya bali ni matokeo ya mipango madhubuti iliyowekwa na Rais.
“Tunapofika kwa wananchi wetu tunapaswa kuisemea Serikali, kwa sababu Serikali inafanya mambo mengi mazuri. Ni wajibu wetu kuyaeleza na kuyatetea haya mema,” amesema Mh. Timoth.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.