#HABARI: Serikali imesema miradi yote yenye thamani ya chini ya shilingi bilioni hamsini inapaswa kutekelezwa na wakandarasi wazawa ili kuwajengea uwezo na kuongeza ushiriki wao katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba wakati wa ziara ya bodi ya wakurugenzi ya PPRA kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya pete (Ring Road) jijini Dodoma.
Simba amesema wasimamizi wa miradi mbalimbali ya ujenzi nchini wana wajibu wa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma, inayotaka wakandarasi wazawa kupewa kipaumbele katika miradi yote iliyo chini ya Sh50 bilioni.
Amesisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuwapa nafasi wakandarasi wa ndani kutekeleza miradi iliyo ndani ya uwezo wao, hatua itakayosaidia kukuza sekta ya ujenzi, kuongeza ajira na kuchochea uchumi wa ndani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania