#HABARI: Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, akiwa ametembelea eneo la kongani ya viwanda ya BUZWAGI Kahama (Buzwagi Special Economic zone), amewasihi wawekezaji wazawa kutumia fursa hiyo kuwekeza katika eneo hilo, ambalo Serikali imedhamiria liwe kitovu cha usambazaji wa bidhaa za migodini kusini mwa jangwa la sahara.
Waziri Mavunde amesema kwa sasa makampuni 15 kati ya makampuni 30 ambayo yametia nia kuwekeza katika eneo hilo, tayari yameanza hatua za awali za kujenga viwanda ikiwemo kampuni ya TEMBO NICKEL, ambayo tayari imeshaanza kuweka miundombinu kwa ajili ya ujenzi.
Hata hivyo, Mavunde amesema Serikali imeelekeza suala la Local Content, kwa mwekezaji yeyote anayewekeza kwenye eneo hilo, lengo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wananufaika na raslimali za nchi yao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.