#HABARI: Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewataka wakandarasi kuweka kipaumbele utu na kuondoa kero kwa wananchi kila wanapopewa kazi za ujenzi hapa nchini kwani huo ndiyo mwelekeo wa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza mkoani Ruvuma jana, Ulega amesema kila kwenye kazi ya ujenzi, ni muhimu kwa mkandarasi kufanya kwanza mambo yatakayorahisisha maisha ya watu na kulinda utu wao badala ya kufikiria tu kumaliza ujenzi wa barabara.
“Kama umepewa kazi ya ujenzi, fikiria unawezaje kurahisisha maisha ya watu? Kama unaweza kuweka kalvati kuzuia maji yasiingie kwenye nyumba za watu, weka kwanza kalvati halafu endelea na ujenzi.
“Kama kuna sehemu barabara imekamilika na taa za usiku unazo, weka taa. Kama kuna kitu unaweza kufanya watu wasikae kwenye foleni kabla hujamaliza ujenzi, fanya halafu endelea na ujenzi. Barabara ni utu na lengo liwe wananchi na sio tu kujenga barabara,” alisema Ulega.
Ulega ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kitahi – Amani Makoro – Ruanda hadi Bandari ya Ndumbi (km 85) kwa kiwango cha lami unaotekelezwa na kampuni ya China Railway Seventh Group (CRSG).
Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge huyo wa Jimbo la Mkuranga, alifanya ziara hiyo baada ya maelekezo ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye alionesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo ingawa serikali tayari imemlipa mkandarasi huyo.
Akitoa maelezo yake, Afisa Mwajiri kutoka kampuni ya CRSG Themistocles Rugabela, alimwomba Ulega kumfikishia salamu za kumuomba radhi Waziri Mkuu na kuhusu kasi ndogo ya utekelezaji wa mradi huo na kuahidi kufanya kazi usiku na mchana kukamilisha ujenzi huo kwa kasi na ubora unaotakiwa.
Hapo awali, wananchi wa eneo la Amani Makoro walimuomba Waziri Ulega kutatua kero ya vivuko vya kupita wananchi katika barabara hiyo ili watoto wa shule na wananchi wengine waweze kuvuka kwa urahisi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania