#HABARI:Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewabadilishia makosa watuhumiwa watatu waliokuwa wanashtakiwa kwa uhaini na kuwapa mashtaka ya kuchoma ofisi ya Chama cha Mapinduzi(CCM) ya Kivule Kata ya Majohe wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
Waliobadilishiwa mashtaka ni Mohammed Steven Madea (28), Fredy Samson Chacha (21) na Peter Basoti Chobe (48) ambao wamepewa dhamana huku wakitakiwa kuhudhuria mahakamani kila kesi yao itapotajwa ambapo kesi hiyo itatajwa tena Januari 22, 2026.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka yenye na namba 28997/2025 watuhumiwa hao walitekeleza tukio hilo siku ya Oktoba 30, 2025 majira ya usiku katika eneo la Bwera-Kivule, Kata ya Majohe wilaya ya Ilala Dar Es Salaam.
Hata hivyo washtakiwa hao walikuwa kwenye kesi ya pamoja ya uhaini ambayo ilikuwa na washtakiwa 12 ambapo watatu ndio waliopewa kosa la kuchoma ofisi huku wengine tisa wakirudishwa rumande mpaka Januari 05, 2026 ambapo ndio kesi yao itatajwa kwani upelelezi wa mashtaka yanayowakabili haujakamilika.
Mawakili wa washtakiwa hao ni Paul Kisabo @advocate_kisabo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na William Maduhu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC).
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania