
Ukurasa mmoja wa mitandao ya kijamii unaouza viporo na masalia ya chakula yaliyobaki mikahawani umepata umaarufu mkubwa huko Israel kiasi kwamba kutokana na hali ngumu ya maisha, Wazayuni wengi wanajitokeza kwenye ukurasa huo kununua chakula kilichobaki mikahawani na matunda yaliyoharibika madukani.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, tovuti ya habari ya Ynet imetangaza katika ripoti yake kuhusu hali mbaya ya kimaisha huko Israel na kuandika: Chakula kilichobaki kinauzwa pamoja na saladi iliyokauka au kikapu cha matunda yanayoharibika kwa nusu bei na Wazayuni wanapigana vikumbo kukinunua.
Chombo hicho cha habari cha Israel baada ya hapo kimehoji kwa kusema hivi ni kweli watu hawa ni wanunuzi au ni watu wanaotafuta njia zozote tu alimradi wapunguze njaa zao? Ndani ya ukurasa huo wa Facebook, wamiliki wa maduka wanatangaza na kuuza bidhaa zao za ziada zilizoharibika kwa nusu bei.
Bidhaa hizo kwa kawaida huwekwa kwenye ukurasa huo mwishoni mwa siku, kila siku, huku wasimamizi wa ukurasa huo wakichapisha mapendekezo yao mara kwa mara kuhusu maeneo salama zaidi, masuala ya usafi na maeneo ya bei nafuu na Waisraeli wengi wanatembelea ukurasa huo kila siku.
Hii ni katika hali ambayo baadhi ya maduka ya Israel yanaweka mapunguzo hayo ya bei katika mfumo wa vifurushi ambapo mteja lazima anunue kifurushi kizima bila ya kutaka na bila ya kujali vitu vilivyomo kwenye vifurushi hivyo. Wengi wao hushitukia wamepoteza pesa zao bure.
La kuzingatia hapa ni kwamba, ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa, wakimbizi wengi wa Kizayuni wanaishi katika hali mbaya ya kiuchumi na kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanachama wengi wa ukurasa huo ni wafanyakazi.