
Walinzi wa pwani wa Marekani wamesema meli hiyo inayosafiri kwenye bahari ya Karibia inapeperusha bendera ya uongo na ni miongoni mwa meli za mafuta zilizo chini ya vikwazo vya Marekani.
Iwapo wataikamata, hiyo itakuwa meli ya tatu yenye mafungamano na biashara ya mafuta ya Venezuala — taifa ambalo Washington inalituhumu kufadhili biashara ya dawa za kulevya.
Hapo jana Jumapili, walinzi hao wa pwani waliikamata meli nyingine wanayoituhumu kusafirisha mafuta ya Venezuela,ikiwa ni wiki mbili tangu walipoizuia meli nyingine.
Serikali ya Rais Nicolas Maduro wa Venezuela imezitaja hatua hizo za Marekani kuwa “wizi na uharamia” wa kimataifa.