Wajumbe wa Marekani na Ukraine, katika taarifa ya pamoja siku ya Jumapili, Desemba 21, wamesifu majadiliano “yenye tija na yenye kujenga” yaliyofanyika wakati wa mazungumzo huko Miami. Muda mfupi kabla, Kyiv ilitangaza kwamba wajumbe wa Ukraine watakutana tena huko Florida na wenzao wa Marekani, ambao walikuwa wakikutana kando na mjumbe wa Urusi, kujadili uwezekano wa suluhu la mgogoro nchini Ukraine.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya rais wa Urusi, kupitia mshauri wake wa kidiplomasia Yuri Ushakov, umesema kwamba mkutano wa pande tatu kati ya Urusi, Marekani, na Ukraine “haukupangwa.”

“Katika siku tatu zilizopita huko Florida, ujumbe wa Ukraine umefanya mfululizo wa mikutano yenye tija na yenye kujenga na washirika wake wa Marekani na Ulaya,” imeandikwa kwenye taarifa hiyo, ambayo ilishirikiwa kwenye mtandao wa kijamii X na Steve Witkoff, mjumbe maalum wa Donald Trump, na kuunganishwa na ujumbe wa Ukraine.

“Washauri wakuu wa usalama wa taifa wa Ulaya pia walishiriki katika majadiliano ili kufafanua mbinu ya pamoja ya kimkakati kati ya Ukraine, Marekani, na Ulaya. Mkutano tofauti na wenye kujenga pia ulifanyika katika muundo wa Marekani na Ukraine, ambapo hati nne muhimu zilishughulikiwa: uundaji wa mpango wa pointi 20, kuweka sawa misimamo kwenye mfumo wa uhakikisho wa usalama wa pande nyingi, kuweka sawa misimamo kwenye mfumo wa uhakikisho wa usalama wa Marekani kwa Ukraine, na uundaji wa mpango wa kufufua uchumi na ustawi. Uangalifu maalum uliwekwa kwa ratiba na mfuatano wa hatua zinazofuata. Ukraine inaendelea kujitolea kikamilifu kufikia amani ya haki na ya kudumu,” ameongeza Steve Witkoff.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Mjumbe Maalum wa Marekani Steve Witkoff ameelezea majadiliano kati ya Ukraine, Marekani, na Ulayakama “yenye tija na yenye kujenga.”

Pia Jumapili, Ujumbe wa Marekani, ukiongozwa na Steve Witkoff na Jared Kushner, mkwe wa rais wa Marekani, walikutana na mwakilishi wa Urusi Kirill Dmitriev katika jiji hili la kusini mashariki mwa Marekani. Huu ulikuwa mkutano wao wa pili mwishoni mwa wiki hiii iliyopita. “Majadiliano yanaendelea kwa njia ya kujenga,” mjumbe wa Moscow amesema.

Siku ya Jumamosi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitoa wito kwa Washington kuongeza shinikizo dhidi ya Urusi. “Marekani lazima iweke wazi: ikiwa hakuna njia ya kidiplomasia, basi kutakuwa na shinikizo kamili,” aliwaambia waandishi wa habari, akibainisha kwamba ni Marekani pekee iliyoweza kushawishi Moscow kumaliza mzozo nchini Ukraine, ambao ulianza karibu miaka minne iliyopita.

Kujumuishwa moja kwa moja kwa Ulaya wakati huu ni maendeleo mapya ikilinganishwa na mikutano ya awali iliyofanyika hivi karibuni kati ya Ukraine na Marekani huko Geneva, Miami, na Berlin.

Putin “yuko tayari kwa mazungumzo” na Macron

Siku ya Jumapili, Desemba 21, ofisi ya rais wa Ufaransa umekaribisha matamshi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye alisema yuko “tayari kwa mazungumzo” na mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Siku ya Jumamosi usiku, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema kwamba Vladimir Putin yuko “tayari kwa mazungumzo” na mwenzake wa Ufaransa, ambaye mwenyewe alielezea bayana mwelekeo huo siku ya Ijumaa baada ya mkutano wa kilele wa Ulaya huko Brussels.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *