Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonya kuwa utawala wa Israeli unatekeleza mashambulizi ya “kujidhuru” dhidi ya jumuiya za Wayahudi maeneo mbali mbali duniani ili kuchochea hofu ya chuki dhidi ya Wayahudi.

Akizungumza Jumapili, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi aliongeza Wazayuni wamewaua Wayahudi katika mataifa mengine ili kuzuia Wayahudi kuondoka ‘Israel’ na kukwepa machafuko ya ndanii ya utawala wa Israel.

Akitaja shambulio la kikatili lililotokea katika hafla ya Kiyahudi mjini Sydney, Australia wiki iliyopita, Jenerali Mousavi amesema si mara ya kwanza Wayahudi kulengwa kwa lengo la kuonesha Israel kama mhanga. Amesisitiza kuwa utawala huo umewahi kutekeleza uhalifu wa aina hiyo dhidi ya Wayahudi mara nyingi hapo kabla.

Kauli ya Jenerali Mousavi imekuja baada ya watu wasiopungua 15 kuuawa na kadhaa kujeruhiwa, pale watu wawili wenye silaha walipofyatua risasi katika tamasha la Kiyahudi Sydney wiki iliyopita.

Iran ililaani shambulio hilo ambapo msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Esmaeil Baghaei, alisema: “Kuna ulazima wa kulaani ugaidi na mauaji ya halaiki lazima yalaniwe popote pale kwani ni kinyume cha sheria na ni uhalifu.”

Jenerali Mousavi ameongeza kuwa matukio ya miaka miwili iliyopita yamefichua asili ya kikhalifu ya Marekani na utawala wa Israeli mbele ya macho ya dunia.

Aidha amesisitiza kuwa maadui wa Iran ambao ni wadanganyifu na wachochezi wa vita hawaheshimu sheria yoyote ya kimataifa wala maadili ya binadamu.

Hata hivyo, amebainisha kuwa Iran imechagua njia ya “muqawama na mapambano na kujiimarisha,” ambayo ni “njia ya heshima na uhuru.”

Jenerali Mousavi amehitimisha kwa kusema Majeshi ya Ulinzi ya Iran kwa kushirikiana na taifa la Iran lenye ustahimilivu yatashinda kwa mshikamano na umoja dhidi ya njama zote kwa kufuata mwongozo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *