Maelfu ya mashabiki walikusanyika kwenye dimba la Moulay Abdellah mjini Rabat, kushuhudia ufunguzi wa michuano hiyo 35 ya AFCON, iliyohudhuriwa na Mwanamfalme Moulay Hassan wa Morocco, Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani – FIFA, Gianni Infantino na mwenzake wa Afrika Patrice Motsepe.

Sherehe za ufunguzizilijumuisha onesho la burudani kabambe ya muziki na ngoma za kitamaduni.

Baada ya onesho la ufunguzi, wachezaji wa Morocco Brahim Díaz na Ayoub El Kaabi waliwapa raha mashabiki wa nchi hiyo kwa kupachika wavuni mabao mawili kwa mtungi, yaliyoiacha Commoro ikiburuta mkia kwenye msimamo wa kundi wa A.

Hii leo kutakuwa na michezo mitatu ya makundi ikiwemo ule utakaozikutanisha Misri na Zimbabwe. Wawakilishi wa Afrika Mashariki, timu za Tanzania, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zitacheza mechi zao za kwanza kesho Jumanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *