Haukuwa mchuano mwepesi pale ambapo mashabiki wa nyumbani, akiwemo Mwanamfalme wa Morocco Moulay Hassan, ambaye awali aliwasalimia wachezaji kabla ya mechi kuanza, waliokuwa katika hali ya kukata tamaa huku taifa la visiwa vya Comoro, lililoko nafasi ya 108 duniani, likionesha mchezo wenye ushindani dhidi ya moja ya timu zinazopigiwa upatu kutwaa taji la AFCON kwa wakati huu.
Kipa wa Comoro, Yannick Pandor, aling’aa kwa namna yake pale alopokoa penalti ya mapema iliyopigwa na Soufiane Rahimi. Lakini mchezaji, Brahim Díaz hatimaye akavunja ukimya katika dakika ya 55, na kusababisha shangwe za faraja kote uwanjani, kabla ya El Kaabi kufunga bao la pili katika dakika ya 74.
Furaha ya mwanamfalme wa Morocco
Mwanamfalme, akitazama kutoka kwenye sehemu yake ya kifalme, hakuweza kuficha furaha yake aliposhangilia kwa makofi.
Dhamira ya Morocco kuwa nguvu kubwa ya soka ni jambo la kifamilia. Ilikuwa shauku ya babu wa mwanamfalme, Hassan II, na mfalme wa sasa, Mohammed VI, ambaye amesimamia moja ya miradi mikubwa zaidi ya michezo barani Afrika ili kufanikisha lengo hilo.
Ufalme huo unatarajiwa kuwa mwenyeji mwenza wa Kombe la Dunia la 2030 pamoja na Hispania na Ureno. Abuu Yusufu ambae ni mwandishi wa habari kutoka Tanzania aliyeshuhudia mchuano huo akiwa Rabat hapa anasema Morocco imejenga msingi wa matarajio yao ya kulichukua tena taji hilo.
Mchuano kati ya Misri na Zimbabwe
Lakini anasema hata kwa Comoro itasaidie kuiweka timu hiyo katika nafasi nzuri katika kushiriki mechi zake zijazo.
Hii leo (22.12.2025) kutakuwa na michezo mitatu ya makundi ikiwemo ule utakaozikutanisha Misri na Zimbabwe.
Wawakilishi wa Afrika Mashariki, timu za Tanzania, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zitacheza mechi zao za kwanza kesho Jumanne.