Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Hamis Livembe, amesema Serikali pamoja na Tume ya Maboresho ya Sheria za Kodi zinapaswa kutangaza hadharani matokeo ya kazi ya tume hiyo, akibainisha kuwa muda uliopangwa kwa utekelezaji wa majukumu yake tayari umekwisha.

Livembe ameongeza kuwa wafanyabiashara wana hamu kubwa ya kufahamu mapendekezo ya tume, hususan yale yanayolenga kupunguza mzigo wa kodi na kurahisisha mfumo wa kodi kwa kuzijumlisha kodi mbalimbali.

Amesema ucheleweshaji wa utoaji wa matokeo ulitokana na shughuli za uchaguzi, lakini kwa kuwa uchaguzi umekamilika, hakuna kizuizi kwa tume kurejea kazini na kuwasilisha ripoti yake kwa umma.

Akizungumzia hali ya biashara wakati wa uchaguzi, Livembe amesema changamoto za kiusalama zilijitokeza na kusababisha kupungua kwa wateja katika baadhi ya maeneo ya biashara, hata hivyo hali hiyo ilikuwa ya muda mfupi na biashara zimerejea katika hali ya kawaida baada ya uchaguzi.

✍ Rebecca Mbembela
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *