Mamlaka ya Nigeria imetangaza siku ya Jumapili, Desemba 21, kuachiliwa kwa wanafunzi 130 waliotekwa nyara mnamo Novemba 21 na watu wenye silaha kutoka shule ya Kikatoliki katika Jimbo la Niger, katika sehemu ya kaskazini ya nchi. Mapema mwezi Desemba, takriban wanafunzi wengine 100 waliotekwa nyara mwezi Novemba walachiliwa. Kulingana na msemaji wa rais, hakuna hata mmoja wa wanafunzi waliotekwa nyara mnamo Novemba 21 ambaye bado anashikiliwa mateka.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Twitter kutoka kwa msemaji wa rais wa Nigeria ulijumuisha picha ya watoto waliokuwa wakitabasamu nyuma ya basi dogo. Kulingana na Sunday Dare, ni miongoni mwa watoto 130 wa shule waliotekwa nyara usiku wa Novemba 21 kutoka kwenye bweni la Shule ya St. Mary’s katika kijiji cha mbali cha Papiri, kaskazini mwa Nigeria.

“Wanafunzi wengine 130 waliotekwa nyara katika Jimbo la Niger wameachiliwa; hakuna mwanafunzi hata mmoja anayeshikiliwa mateka,” msemaji wa rais alitangaza siku ya Jumapili, akimaanisha kuachiliwa kwa awali kwa watoto wapatao 100 waliotekwa nyara kutoka shule hiyo hiyo.

Kulingana na chanzo cha Umoja wa Mataifa kilichonukuliwa na shirika la habari la AFP, watoto wa shule watahamishiwa Minna siku ya Jumatatu, mji mkuu wa Jimbo la Niger.

Kulingana na Chama cha Wakristo nchini Nigeria, wanafunzi 315 na wafanyakazi walitekwa nyara mnamo Novemba 21. Karibu 50 kati yao waliweza kuwatoroka watekaji wao muda mfupi baadaye.

Baada ya kuachiliwa kwa takriban wanafunzi 100 mnamo Desemba 7, watu wapatao 165 walikuwa bado hawajapatikana, kulingana na takwimu zilizotolewa na dayosisi ambayo Shule ya St. Mary’s iko. Kwa upande wake, Rais wa Nigeria Bola Tinubu aliripoti kwamba watu 115 walikuwa wakishikiliwa na watekaji nyara wao.

Wakati huo huo, chanzo cha Umoja wa Mataifa kumelieleza shirika la habari la AFP kwamba wale wote waliotekwa nyara mnamo Novemba 21 wamechiliwa. Dazeni kadhaa kati yao, ambao waliaminika kuwa bado wameshikiliwa mateka, kwa kweli walifanikiwa kutoroka wakati wa shambulio hilo na kurudi nyumbani.

Utambulisho wao haujafichuliwa, na maelezo ya kuachiliwa kwa watoto hayajawekwa wazi.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Nigeria cha Arise News, kikinukuu chanzo cha usalama, “kuachiliwa huku ni matokeo ya shinikizo endelevu la usalama na juhudi zilizoratibiwa, huku kukiwa na wito unaoongezeka wa ulinzi zaidi wa shule na hatua madhubuti za kuzuia mashambulizi kama hayo kujirudia.” Toleo hili la matukio linapingwa na baadhi ya wachambuzi waliohojiwa na AFP, ambao wanapendekeza fidia ililipwa, kitendo ambacho kimepigwa marufuku na sheria nchini Nigeria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *