Wizara ya Ulinzi ya Cambodia imesema masaa machache baada ya mazungumzo ya usuluhishi yaliyofanyika Malaysia, jeshi la Thailand lilianza kushambulia kwa mabomu maeneo ya Siem Reap na Preah Vihear.

Siem Reap ndiko makao makuu ya hekalu maarufu la Angkor nchini Cambodia ambalo turathi ya shirika la kimataifa la UNESCO.

Jeshi la Thailand kwa upande wake limesema Cambodia iliwafyatulia maroketi kadhaa hii leo, na kufanya jeshi lake kujibu kwa mashambulizi hayo ya anga kwenye kambi mbili za kijeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *