Venezuela, baada ya kuvuka kikwazo cha vikwazo vya kiuchumi, imejinyakulia kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi katika Amerika ya Kusini mwaka 2025.
Huku Marekani ikijaribu kuisambaratisha Venezuela kwa kuendeleza vikwazo vikali visivyo halali, kuizingira kiuchumi na sasa hata kutishia mashambulizi ya kijeshi, Tume ya Kiuchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Amerika ya Latini na Karibea (CEPAL) katika ripoti iliyowashangaza sana Wamagharibi, imetangaza kuwa Venezuela, licha ya vikwazo hivyo, imesajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi katika Amerika ya Kusini mwaka 2025.
Taasisi hii iliyo chini ya Umoja wa Mataifa, ilipotangaza tathmini ya awali ya uchumi wa nchi za eneo, imethibitisha kushindwa kwa siasa za shinikizo la juu za Marekani dhidi ya Venezuela. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Venezuela imeandikisha ukuaji wa asilimia 6.5 mwaka 2025 na kusimama kileleni mwa jedwali la ukuaji wa uchumi Amerika ya Latini na Karibea . Ripoti hii ni ushahidi dhahiri wa ushindi wa mfano wa “uchumi wa kimuqawama” au kimapamban wa serikali ya Kibolivaria dhidi ya ubeberu.
Ripoti hii inabainisha kuwa Venezuela mwaka 2024 pia ilipiga hatua kubwa kwa ukuaji wa asilimia 8.5, na kuendeleza mwenendo huo mwaka 2025 kwa asilimia 6.5. Hali hii imeiweka mbali sana na wastani wa ukuaji wa kikanda ambao ni kati ya asilimia 2.3 hadi 2.4 pekee. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa uchumi wa Venezuela si tu umesimama imara dhidi ya njama za kibeberu, bali pia uko katika hatua ya kustawi upya.
Sehemu nyingine ya ripoti ya CEPAL, inayobatilisha propaganda za vyombo vya habari vya Magharibi, imeangazia mafanikio ya serikali ya Nicolás Maduro katika kudhibiti mfumuko wa bei. Taasisi hii ya kimataifa imekiri kwamba mfumuko wa bei nchini Venezuela, nchi ambayo inajulikana kwa itikadi yake ya ujamaa, umepungua kwa zaidi ya asilimia 87 ndani ya mwaka mmoja. Venezuela imefanikiwa kutoka katika hali ya mfumuko wa bei mkubwa, uliotokana na vita vya kifedha vilivyopangwa na maadui wa taifa hilo, na kufikia kiwango cha mfumuko wa bei kinachoweza kudhibitiwa; mafanikio haya yanachukuliwa kuwa moja ya ushindi muhimu zaidi wa kiuchumi katika miaka ya hivi karibuni.
Kwa kuzingatia ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa, inapaswa kusemwa kwamba Venezuela imeweza kujitokeza kama kinara wa ukuaji wa uchumi katika Amerika ya Latini na Karibea. Moja ya sababu kuu za ustawi hii ni kupungua kwa kiasi kikubwa kwa mfumuko wa bei. Venezuela, ambayo kwa miaka mingi ilihangaika na janga la mfumuko wa bei mkubwa, imefanikiwa ndani ya mwaka mmoja kupunguza mfumuko wa bei kwa zaidi ya asilimia 87 na kuufikisha katika kiwango kinachoweza kudhibitiwa. Mafanikio haya makubwa yameleta uthabiti wa kiasi katika soko la ndani na kuweka mazingira bora kwa ukuaji wa uzalishaji na uwekezaji.
Sababu nyingine ni ongezeko la uzalishaji wa mafuta na nishati. Licha ya vikwazo vya nje, serikali ya Venezuela imeweza kurejesha sehemu ya uwezo wake wa mafuta na kuongeza mauzo ya nishati nje ya nchi. Hatua hii imeiletea taifa mapato zaidi ya fedha za kigeni, na kuchangia kuimarisha akiba ya fedha za kigeni pamoja na kufadhili miradi ya ndani.

Aidha, utofauti wa uchumi kupitia kuunga mkono sekta za kilimo, viwanda na huduma umechukua nafasi muhimu katika ukuaji huu. Sekta binafsi na ya umma, licha ya vizuizi vilivyotokana na vikwazo, zimewekeza upya katika uzalishaji wa ndani. Juhudi hizi zimepunguza utegemezi wa kipekee kwa mafuta na kufanya sekta nyingine pia kuchangia kwa kiwango kikubwa katika ukuaji wa uchumi.
Kutoka katika mtazamo wa kijamii, kupungua kwa mfumuko wa bei na kuongezeka kwa uzalishaji kumeleta maboresho ya kiasi katika hali ya maisha ya wananchi. Ingawa changamoto za kimuundo bado zipo, uthabiti wa kiuchumi umeweza kujenga imani fulani ndani ya jamii na kuweka mazingira ya kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza nafasi za kazi.
Katika ngazi ya kikanda, utendaji wa Venezuela unapata uzito zaidi hasa ikizingatiwa kuwa mataifa mengi ya Amerika ya Kusini yanakabiliwa na ukuaji mdogo na mdororo wa uchumi. Wakati uchumi mkubwa kama Brazil na Chile umekua kwa takribani asilimia 2.5 pekee, Venezuela kwa ukuaji zaidi ya mara mbili ya wastani wa kikanda imeweza kujipatia nafasi ya kipekee.
Kwa jumla, Venezuela kupitia mchanganyiko wa kupunguza mfumuko wa bei, kuongeza uzalishaji wa mafuta, kuimarishwa sekta mbali mbali uchumi na uwekezaji wa ndani, imeweza katika miaka ya hivi karibuni kujitokeza kama kinara wa ukuaji wa uchumi katika eneo la Amerika ya Kusini na Karibea.. Mafanikio haya yanapata umuhimu maalum katika mazingira ya mdororo wa kikanda, ingawa kuendeleza mwenendo huu kunahitaji marekebisho ya kimuundo na kuondolewa kwa vizuizi vya nje.
Inaonekana kwamba serikali ya Trump, ambayo kama ilivyokuwa kwa tawala zilizopita za Marekani imeweka mkazo wake katika kudhoofisha na hatimaye kuangusha serikali ya mrengo wa kushoto ya Venezuela na pia Rais Nicolás Maduro, imepatwa na mshtuko mkubwa zaidi kutokana na ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu ukuaji wa kiuchumi wa kushangaza wa Venezuela.