
Washington inaendeleza kizuizi chake kwenye mafuta ya Venezuela. Baada ya kuizuia meli ya pili ya mafuta mwishoni mwa wiki hiii iliyopita huko Karibiani, Marekani imefuatilia meli ya tatu siku ya Jumapili, Desemba 21.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Caracas inalaani hatua hizo za Marekani na kuzitaja kama “wizi” na kitendo cha “uharamia wa majini,” ingawa meli ya mafuta iliyokamatwa haiko kwenye orodha ya vyombo vilivyochukuliwa vikwazo na Wizara ya Fedha ya Marekani. Mojawapo ya sababu za kizuizi hiki ni kudhibiti vyema uzalishaji wa mafuta wa Venezuela.
“Walinzi wa Pwani wa Marekani wanafuatilia kikamilifu meli iliyo chini ya vikwazo (…) ambayo inashiriki katika kukwepa vikwazo kinyume cha sheria vilivyokwa dhidi ya Venezuela. Inasafiri chini ya bendera ya uwongo na iko chini ya amri ya mahakama ya kukamatwa,” afisa wa Marekani ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina. Alikuwa akithibitisha ripoti za vyombo vya habari.
Iwapo wataikamata, hiyo itakuwa meli ya tatu yenye mafungamano na biashara ya mafuta ya Venezuala — taifa ambalo Washington inalituhumu kufadhili biashara ya dawa za kulevya.
Siku ya Jumanne, Desemba 16, Marekani ilitangaza, kuwekwa kwa kizuizi cha majini kuzunguka Venezuela, nchi inayoongozwa na Nicolas Maduro, ikilenga meli za mafuta zinazodaiwa kuwa chini ya vikwazo. Tayari wamekamata meli mbili zinazoshukiwa na Washington kusafirisha mafuta ya Venezuela chini ya vikwazo.