Wakulima wa jimbo la Isimani mkoani Iringa wameiomba serikali kuwapatia mbegu za muda mfupi, hususan za mahindi na mpunga, baada ya mazao yao kukauka kutokana na ukosefu wa mvua za kutosha.
Ombi hilo limetolewa katika kata ya Mahuninga, yenye wakazi wapatao 4,994, ambapo wengi wao hutegemea kilimo na ufugaji kwa maisha yao ya kila siku.
Wakulima wanasema kuchelewa kwa mvua kumesababisha hasara kubwa na wanaiomba serikali kuchukua hatua za haraka ili kuokoa msimu wa kilimo na kulinda usalama wa chakula katika eneo hilo.
Mohammad Nyaulingo
Mhariri | @claud_jm
#UTV108 #AzamTVUpdates #AdhuhuriLive